Tuesday, 24 October 2017

Fahamu uwezo wa chungwa kwenye matatizo haya ya kiafya


oranges-and-pregnancy
Chungwa ni moja ya tunda ambalo linasifika kwa kuwa na ladha nzuri pamoja na virutubisho kadhaa ikiwa ni pamoja na vitamin C.

Miongoni mwa virutubisho vingine vinavyopatikana ndani ya chungwa ni pamoja na vitamin B, B2, B2,B3,B5 na B6 ambazo zote ni muhimu kwa utendaji bora wa mwili.

Mfano vitamin B1 yenyewe kazi yake kubwa ni kusaidia kurejesha seli mpya za mwili zilizoharibika, huku vitamin B2 yenyewe ikijikita katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu mwilini.

Vitamin B3, yenyewe husaidia mwili kutengeneza cholesterol nzuri ndani ya mwili

Chungwa pia huongeza nyuzinyuzi ndani ya mwili na inaelezwa kuwa chungwa kubwa lina asilimia 18 ya nyuzinyuzi zinazohitajika kwa mahitaji ya kila siku.

Tunda hili pia ni muhimu kwa uboreshaji wa afya ya mifupa hii ni kutokana na kuwa na madini ya  calcium, vitamin D , K  na vitamin B12 ambazo zote husaidia kulinda afya ya mifupa na kuifanya kuimarika.

Chungwa pia hulinda afya ya ini kutokana na kuwa na vitamin C nyingi ambayo huwa na manufaa pia kwa afya kiungo hicho muhimu ndani ya mwili.

Tunda hili pia husifika kuboresha afya ya umeng'enyaji wa chakula pamoja kupunguza maumivu ya viungo na mtu anayetumia tunda hili huweza kupunguza uwezekano wa kuwa na uzito mkubwa.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment