Tuesday, 10 October 2017

Faida za juisi ya tende kiafyaIkitokea ukaandaa mchanganyiko wa tende na tufaa (apple) na kupata juisi yake huenda ikakusaidia kwa matatizo kadhaa ya kiafya au kuimarisha afya yako pia.

Ndani ya mchanganyiko huo kuna virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini ya chuma, potassium, magnesium, n,k Vingine ni pamoja na vitamini B1,B2, B6.

Kutokana na uwepo wa vitu hivyo ndani ya mchanganyiko huo kuna ufanya mchanganyiko huo kusaidia kuongeza mzunguko wa damu ndani ya mwili.

Aidha, uwepo wa madini ya potassium ndani ya mchanganyiko huo unafanya juisi hiyo kuwa na msaada wa kuondoa mlundikano wa mafuta mabaya mwilini. (cholesterol)

Pia ndani ya mchanganyiko wa tende na tufaa kuna madini ya chokaa ambayo husaidia kuimarisha afya ya moyo kwa kuimarisha misuli yake.

Pamoja na hayo, juisi yenye mchanganyiko wa tende na tufaa husaidia kulinda afya ya figo na kuifanya kuwa na uwezo mzuri wa kufanya kazi zake ndani ya mwili.

Ili kunufaika na juisi hii unashauriwa kujenga utaratibu wa kunywa kinywaji hicho angalau mara 2 kwa kila wiki.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua tufaa na ulioshe vizuri kisha likate vipande vidogo vidogo halafu chukua tende kiasi cha kiganja kimoja cha mkono na uziondoe mbegu zake halafu changanya pamoja na vipande vya tufaa kwenye blenda na changanya maziwa kidogo kisha tumia mchanganyiko huo kunywa

Kumbuka kuwa hivi karibuni kwa wewe mzanzibar tutakuwa karibu nawe pale Magomeni ambapo tunataraji kufungua tawi letu

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment