Wednesday, 18 October 2017

Hizi hapa faida za hiliki zitakazokusaidia kujenga afya yako


Hapa duniani Mwenyezi Mungu ametujalia vitu mbalimbali ambavyo vikitumika vizuri huweza kuwa na thamani sana katika maisha yetu ya kila siku hususani katika kujenga afya zetu pia.

Hiliki ni moja ya kiungo ambacho wengi wetu tunakifahamu sana na huenda huwa tunakitumia karibu kila siku kwenye shughuli za mapishi ya jikoni hususani katika kuandaa chai, lakini hiki si kiungo pekee bali huambatana na faida zake kiafya.

Matumizi ya hiliki husaidia sana kuipa uwezo mzuri figo wa kuondoa taka mwili ndani ya mwili, huku ikisaidia kuweka sawa mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni, kuondoa kiungulia, gesi tumboni pamoja na kuwasaidia wale wenye shida ya kukosa choo kwa muda mrefu.

Aidha, hiliki imekuwa ikisifika kwa uwezo wake wa kusaidia kuweka sawa harufu ya kinywa, pamoja na kutibu shida ya vidonda vya mdomoni pamoja na matatizo yote ya kinywa na koo.

Pia kiungo hiki huweza kuwasaidia wenye maambukizi kwenye njia ya mkojo, matatizo ya figo na kibofu cha mkojo, sambamba na kupambana na magonjwa mbalimbali.

Hiliki pia inauwezo wa kukabilina na hali ya maambukizi ya mafua sambamba na kikohozi, huku ikisifika kwa kuwa na uwezo wa kuimaimarisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula pamoja na kuondoa maumivu ya viungo mwilini.

Halikadhalika hiliki inasifika pia kwa uwezo wake wa kusaidia kulinda afya ya kibofu cha mkojo pamoja na ini pia

Mbali na hayo, hiliki pia inauwezo mzuri wa kukabiliana na matatizo ya saratani, pamoja na presha.

Unaweza kuwasiliana nasi pia kama unahitaji kujua masuala mbalimbali kuhusu lishe bora kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment