Wednesday, 11 October 2017

Hizi hapa faida za kijiko kimoja cha tangawizi na binzari


Tangawizi na binzari ni miongoni mwa viungo ambavyo mara kadhaa tumekuwa tukivizungumzia kuhusu manufaa yake kiafya.

Lakini hatujawahi kuzungumzia faida zinazoweza kupatikana endapo viungo hivyo viwili vitachanganywa pamoja.

Hivyo leo msomaji wangu naomba nikueleze kuwa, tangawizi na binzari au manjano kama wengine wanavyoifahamu zikichanganywa pamoja huweza kusaidia haya yafuatayo:-

1. Huweza kudhibiti tatizo la kisukari
Uwezo wa viungo hivi vinapounganishwa kwa pamoja husaidai kudhibiti dalili za ugonjwa wa kisukari.

2. Huboresha kinga za mwili
Mchanganyiko huo unauwezo wa kuongeza uimara wa kinga za mwili na kupambana na maambukizi kadhaa inaweza kuwa kama anti- fungal, anti- bacterial n.k

Aidha, mchanganyiko huo pia husaidia kuponya matatizo ya kikohozi, homa , na kuondoa uchovu wa mwili pia.

3. Hulinda ngozi.
Mchanganyiko wa binzari na tangawizi husaidia kuboresha afya ya ngozi kutokana na uwezo wake wa kuhamasisha ukuaji wa seli mpya ndani ya mwili.

Pia mchanganyiko huu husaidai kupunguza mikunjo ya ngozi na kuilinda ngozi dhidi ya chunusi na  maambukizi kadhaa ya bakteria.

Zingatia
Ni vyema kuwasiliana nasi kabla ya kuandaa mchanganyiko huo ili kupata ufafanuzi wa kina zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 nasi tutakuelekeza.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment