Tuesday, 10 October 2017

Ifahamu kazi ya mafuta ya maboga


Tatizo la upotevu wa nywele (kukatika) ni tatizo ambalo huwakumba baadhi ya watu na kuwakosesha raha kabisa, hivyo leo nimeona ni vyema tuzungumzia tatizo la upotevu wa nywele.

Kimsingi tatizo hili huja pale ambapo nafasi ya nywele zinazoondoka pasipo kuzibwa upya.

Kipara ni moja ya matatizo ambayo yanawakumba wanaume tangu hapo kale kutokana na ukosefu wa nywele.

Hata hivyo, kunaweza kuwa na sababu mbalimbali zinazosababisha upotevu wa nywele kwa wanawake na wanaume.

Baadhi ya sababu ni pamoja na utumiaji wa madawa kiholela, kumalizika kwa kipindi cha uzazi kwa wanawake (yaani menopause), upungufu wa madini ya chuma na zinki, upungufu wa protini, kunywa pombe na uvutaji tumbaku.

Leo naomba nikwambie hii njia mojawapo ambayo huweza kupunguza tatizo hilo la kutoweka kwa nywele yaani kipara.

Njia hiyo ni pamoja na kutumia mafuta ya mbegu za maboga ambayo unachopaswa kufanya ni kupata mafuta hayo kisha mhusika atatumia mafuta hayo kupaka kichwani mara mbili kwa wiki.

Mafuta hayo ni vyema yapakwe usiku na mhusika kulala nayo hadi asubuhi kisha kuosha kichwa chake asubuhi yake.

Pamoja na hayo, unashauriwa kupata ushauri zaidi kutoka kwa wataalam kabla ya kuanza kutumia mbinu hii.

Kwa maelezo zaidi au msaada unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu somo hili unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment