Friday, 27 October 2017

Je, unalifahamu tunda la shelisheli? zipo hapa faida zake


Tunda la shelisheli ni zao kuu maeneo ya Pasifiki na lina kiwango kikubwa cha wanga na huweza kuliwa likiwa bichi au baada ya kupikwa.

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 na huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50.

Tunda hili lina faida mbalimbali zikiwemo za kiafya na za kiuchumi, lakini moja ya sifa kuu ya tunda hili ni kuwa na kiwango kizuri cha wanga.

Kutokana na kiwango kikubwa cha wanga kwenye shelisheli kunalifanya tunda hilo kutumika badala ya unga wa ngano kwenye baadhi ya nchi na hivyo hutengenezewa chapati.

Aidha, utomvu wake unaelezwa kutumika kama njia asili ya kupunguza matatizo ya kuhara na magonjwa ya ngozi. 

Mbali na hayo, maua ya mshelisheli yanapochomwa moshi wake husaidia kufukuza mbu, na mti wake hufaa kwa matumizi ya mbao za ujenzi wa nyumba na mashua kwani ni thabiti dhidi ya mchwa. 

Kama unaswali, maoni au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment