Monday, 2 October 2017

Kifahamu kinywaji chenye uwezo wa kukata kitambi haraka


Kuwa na uzito mkubwa (kitambi) ni moja ya kikwazo kwa wengi ambao hujikuta katika muonekano huo.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali hali ya kuwa na kitambi mara nyingi huweza kuambatana na magonjwa kadhaa kama vile kisukari (diabetes type 2).

Pia kitambi huwa na uhusiano wa karibu na mgaonjwa kama vile  presha na matatizo ya umoyo kwa ujumla.

Hivyo ni vyema kuepukana kuwa na kitambi kutokana na madhara ambayo huweza kuambatana na hali hiyo.

Hata hivyo, unaweza kutumia lishe mbalimbali maaluma zenye uwezo wa kuondoa hali ya kitambi, lakini leo naomba kukueleza moja ya kinywaji ambacho huweza kupunguza kitambi au kumaliza kabisa.

Jinsi ya Kuandaa kwa matumizi ya mtu mmoja
Unatakiwa kupata tango moja lenye ukubwa wa wastani, nusu kipande cha limao, majani ya kotimiri (parsley)  fungu moja na tangawizi kipande kimoja.

Baada ya hapo vioshe vizuri na kisha viweke vyote kwenye mashine ya kusagia juisi blender na uvisage kwa pamoja, isipokuwa kipande cha limao ambacho utakikamulia baada ya kusaga yale mahitaji mengine. Kisha chuja na upate juisi yake.

Juisi hiyo utakuwa unakunywa usiku kabla ya kulala kila siku kwa muda wa wiki tatu hadi nne mfululizo.

Kwa maelezo zaidi au ushauri kuhusu lishe bora na asili unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment