Monday, 23 October 2017

Kinywaji cha mbogamboga chenye kupunguza madhara ya vidonda vya tumbo


Vidonda vya tumbo ni matokeo ya uzalishaji wa tindikali aina ya haidrokroliki asidi nyingi kuliko kiasi ndani ya tumbo, ambayo huchangia uharibifu wa utando wa ngozi nyembembe ndani ya utumbo kubwa na tumbo dogo.

Zipo dalili kadhaa za tatizo hili ambazo huainishwa na wataalam wa afya ambazo ni pamoja na maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo, ambayo mara nyingi hutokea saa chache kabla ya kula.

Pia wataalam wanaeleza kuwa miongoni mwa chanzo cha tatizo hilo ni pamoja kula vyakula vilivyokolezwa viungo, kutokuwa na muda maalum wa kula, msongo wa mawazo na mengine kadhaa ambayo si rahisi kuyaainisha yote.

Sasa hapa naomba kukueleza msomaji wangu kuwa moja ya njia ya kupunguza madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na kutumia juisi ya mbogamboga. ni vyema kutumia juisi mara kwa mara.

Unaweza kuandaa juisi ya spinachi, karoti kwa pamoja au juisi ya karoti na matango kwa pamoja kisha ukapata glasi moja kila siku na ukajikuta ukipata ahueni zaidi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment