Monday, 2 October 2017

Kitakachotokea kwenye afya yako endapo utakula ndizi 2 kila siku


Ndizi ni moja ya matunda yenye ladha nzuri na faida mbalimbali za kiafya kwa mtumiaji wa tunda hilo.

Kuna faida nyingi zinazotokana na tunda hili lakini leo nitakwambia faida kadhaa ambazo huweza kutokea kwa mtu ambaye anakula ndizi mbili kila siku.

1. Ni tunda nzuri kwa afya ya moyo
Ndizi zina kiwango kidogo cha madini ya 'sodium', lakini zina wingi wa madini ya potassium, ambayo husaidia kurekebisha msukumo wa damu ndani ya  mwili na kuboresha afya ya moyo. Hivyo ni vyema kula ndizi mbili kila siku ili kunufaika na tunda hili.

2. Suluhisho na kukosa choo
Unapotumia tunda hili kila siku ndizi mbili si rahisi kwako kupatwa na shida ya kukosa choo kutokana na tunda hili kuwa na kiwango kizuri cha nyuzinyuzi.

3. Huongeza nguvu mwilini
Ndizi zina kiwango kizuri cha madini, vitamini na kabohydrate ambavyo ni vyanzo vizuri vya nishati mwilini,  lakini pia uhakikisha usalama wa misuli yako.

4. Ni kinga ya tatizo la anemia
Ulaji wa ndizi huweza kumsaidia mhusika kuepuka shida ya anemia kutokana na tunda hilo kuwa na kiwango kizuri cha madini ya chuma. Hivyo hufaa kutumia mara kwa mara angalau kila siku ndizi 2,

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment