Friday, 27 October 2017

Kitunguu swaumu huweza kutoa msaada kwa afya yako


Shinikizo la damu (presha) kitaalam huitwa 'Hypertension' kwa jina la kawaida shinikizo la damu.

Shinikizo la damu kwa kawaida hutokea endapo msukumo wa damu katika kuta za mishipa ya damu unapoongezeka kutokana na mishipa ya kusafirisha damu kuziba au kuwa midogo na kushindwa kupitisha damu kama inavyotakiwa.

Hali hiyo husababisha moyo kufanye kazi zaidi kuliko kawaida ili kuzungusha damu mwilini.

Mara nyingi ugonjwa huu huwa hauna dalili za moja kwa moja, lakini baadhi ya watu wenye shinikizo la damu la juu hupata maumivu ya kichwa hasa upande wa nyuma ya kichwa hasa asubuhi, wengine huisi kizunguzungu nk.

Hata hivyo zipo njia za kuepuka ugonjwa huu ambazo ni pamoja na kubadilisha mfumo wa maisha. Ikiwa ni pamoja na kuzingatia ulaji bora wa chakula hasa vyakula vya asili pamoja na kufanya mazoezi,.

Mgonjwa wa shinikizo la damu la juu hupaswa kuepuka kula chumvi na mengine ambayo atashauriwa na daktari.

Kitunguu swaumu ni moja ya kiungo ambacho huweza kutoa ahueni kwa mtu mwenye tatizo la presha.

Unachopaswa kufanya ni kupata punje 5 za kitunguu swaumu na uchanganye na maji lita moja kisha chemsha maji hayo yakiwa pamoja na kitunguu swaumu.

Baada ya kuchemka vizuri yaache maji hayo yapoe, kisha mhusika yaani yule mtu mwenye tatizo la presha atumie mchanganyiko huo ndani ya wiki 3 hadi 4 mfululizo. Kwa maelezo ya kina zaidi kuhusu njia hii ni vyema uwasiliane nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment