Monday, 30 October 2017

Mafuta ya mzaituni hutoa ahueni kwa wenye kisukari


Mzaituni ni mti unaostawi katika mataifa mbalimbali duniani, lakini zaidi huweza kustawi zaidi nchini Israel.

Mti huu ambao umetajwa mara kadhaa katika vitabu vya dini pia unaelezwa kuwa na uwezo wa kutoa ahueni kwa matatizo kadhaa ya kiafya.

Aidha, mafuta yatokanayo na mzaituni huweza kuponya maumivu ya kichwa ya mara kwa mara endapo mhusika atapaka mafuta hayo baada ya kunyoa nywele zake.

Aidha, kwa wale wanawake wenye shida ya kutokwa na maji yenye harufu sehemu za siri huweza kutumia majani yake na kumaliza shida hiyo.

Faida nyingine za mzaituni ni pamoja na kulinda afya ya ngozi ambapo hulainisha ngozi na kuifanya kuonekana vizuri kutokana na kuwa vitamin A, D, E na K ambazo husaidia kuondoa sumu kwenye ngozi.

Mafuta ya mzaituni pia husaidia kutuliza maumivu ya tumbo na mafua, ambapo mhusika atapaswa kupaka mafuta hayo kati ya tundu moja la pua na jingine mara tatu kwa siku.

Pamoja na hayo, mafuta ya mzaituni pia huondoa shida ya ganzi miguuni au mikononi endapo mafuta hayo yatatumika kuchua sehemu zenye shida hususani kutwa mara mbili kwa kila siku yaani asubuhi na jioni.

Pia mafuta ya mzaituni hutuliza maumivu ya sikio, ambapo mhusika atahitajika kupasha kidogo mafuta hayo na kuwa na joto la wastani, kisha baadaye kudondoshea matone matatu ya mafuta hayo kwenye sikio lenye maumivu. Fanya zoezi hilo asubuhi na jioni kabla ya kulala kwa muda wa siku 3.

Mafuta ya mzaituni pia huweza kupambana na aina mbalimbali ya bakteria na miongoni mwa bakteria ambao huweza kdhurika na mafuta haya ni bakteria aina ya 'Helicobacter Pylori', ambao huishi tumboni na husababisha tatizo la vidonda vya tumbo.

Mlo unaoandaliwa kwa mchanganyiko wenye mafuta ya mzaituni huwa na manufaa kwa watu wenye kisukari kwani huwasaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa kwenye jarida la 'The American Journal of Clinical Nutrition' walibaini kuwa matumizi ya mafuta haya hupunguza hatari ya kukumbwa na kisukari hususani kwa wanawake.

Mafuta ya mzaituni pia hushusha kiwango cha sumu mwilini (cholestrol ) kutokana na kuwa na kiwango cha wastani cha mafuta yaitwayo 'saturated' na 'polynsaturated' hali hiyo inachangia mafuta hayo kuwa na uwezo wa kudhibiti kiwango cha sumu kwenye mwili, lakini pia mafuta haya yanakiwango cha asilimia 75 hadi 80 ya mafuta mazuri kwa afya ya miili yetu.

Mbali na hayo, mafuta haya huwafaa zaidi wenye shida ya kukosa choo kutokana na uwezo wake wa kurekebisha mmeng'enyo wa chakula tumboni na hivyo kusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Kama unaswali, maoni au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment