Tuesday, 10 October 2017

Majani ya ukwaju huondoa tatizo la tetekuwanga

Tetekuwanga ni miongoni mwa magonjwa ambayo huambukizwa kwa urahisi sana kati ya mtu mmoja hadi mwingine.

Ugonjwa huu husababishwa na virusi viitwavyo 'varicella-zoster ' na mhusika huweza kuwaambukiza wengine endapo atagusana na mtu ambaye hajaathirika au hata kupitia njia ya hewa pia.

Kwa kawaida mtu ambaye amepatwa na maambukizi ya ugonjwa huu huweza kuona dalili ndani ya siku 10 hadi 21 ambapo ngozi huanza kutoka kama vipele au vipele vidogo vidogo.

Majani ya ukwaju ni miongoni mwa njia za asili ambazo huweza kutatua tatizo hili kwa wale wenye shida ya tetekuwanga.

Unachopaswa kufanya ni kupata majani ya ukwaju kisha yachemshe halafu tumia majani hayo yaliyochemshwa kupaka sehemu iliyoathirika.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment