Tuesday, 17 October 2017

Makundi ambayo hayashauriwi kutumia tangawizi

Huenda katika soma soma yako sehemu mbalimbali umejikuta ukikutana na ameelezo yanayoeleza kuhusu faida za tangawizi na umuhimu wake.

Sasa leo hapa naomba nikukutanishe na makundi ya watu ambao hawapaswi kutumia kiungo hicho na kwa nini hawatakiwa kutumia.

1. Kinamama wajawazito
Tangawizi inanguvu ambayo huweza kusababisha msukumo wa mama kujifungua mapema hata kabla ya siku za matarajio kutimia.

2. Watu wenye malengo ya kuongeza uzito.
Kama unampango wa kuongeza uzito wa mwili wako basi tangawizi haikufahi kabisa, lakini kama unampango wa kupunguza mwili basi inaweza kuwa moja ya njia ya kukusaidia pia.

3. Watu wenye shida ya kuvuja damu
Kama umekuwa ukisumbuliwa na matatizo ya kutoka damu mfano puani mara kwa mara basi tangawizi utatakiwa kuiepuka na kutotumia kwani hii hufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa mzuri zaidi na hivyo kama unatatizo hilo huweza kukuletea madhara.

4. Watoto wadogo pia si vizuri kutumia tangawizi

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment