Friday, 13 October 2017

Mambo 10 yanayoweza kufanywa na juisi peazi kwenye mwili wako


Peazi ni tunda lenye ladha nzuri na mara nyingi huwa na rangi ya kijani, huku ndani likiwa na rangi nyeupe.

Tunda hili limesheheni virutubisho kadhaa ikiwa ni pamoja na nyuzinyuzi, lakini pia huweza kuwa na manufaa zaidi pale linapoandaliwa kama kinywaji (juisi).

Zifuatazo ni baadhi ya faida ambazo huweza kupatikana kwa mtumiaji wa juisi ya peazi:-

1. Ni kinywaji kizuri kwa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula kama nilivyosema hapo awali kutokana na kuwa na kiwngo kizuri cha nyuzinyuzi.

2. Ni nzuri kwa afya ya moyo, kutokana na kuwa na kiwango cha 'fiber' za kutosha ambazo huwezesha kupunguza kiwango cha cholesterol ndani ya mwili na hivyo kufanya afya ya moyo kuwa salama zaidi.

3. Kinywaji kizuri kwa afya ya mifupa, ndani ya juisi hii kuna kirutubisho kiitwacho 'boron'  ambacho husaidia uvyonzaji mzuri wa madini ya 'calcium', ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa.

4. Kinywaji rafiki kwa kinamama wajawazito, kutokana na kuwa na 'folic acid' kiwango kizuri ambacho husaidia kupunguza madhara wakati wa kujifungua.

5. Juisi ya peasi pia huimarisha mfumo wa upumuaji mwilini na kupunguza madhara ya kikohozi pamoja na dalili za pumu.

6. Huimarisha kinga za mwili, hii ni kutokana na juisi hiyo kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin C na madini ya 'copper' ambayo hufahamika kwa kuwa na uwezo wa kupambana na maambukizi kadhaa ya mwili.

7. Kazi nyingine ya juisi ya peazi ni kusaidia kushusha homa, hivyo huweza kutumiwa pia na watu wenye homa.

8. Pia juisi hii husaidia kupambana na maambukizi ya kwenye ngozi kutokana na kuwa na kirutubisho cha 'antioxidants'  ambayo huweza kupambana na maambukizi kadhaa ya ngozi ikiwemo chunusi.

9. Husaidia kuponya majerahA, uwezo huu unatokana na juisi hiyo kuwa na vitamin K  ndani yake, ambayo kazi yake ni kusaidia kugandisha damu pale mhusika anapopatwa  na jeraha.

10. Juisi hii pia inapendekezwa kwa matumizi ya watoto kwa sababu inakiwango kidogo cha acid.


Kwa ushauri zaidi unaweza kuongea nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment