Monday, 23 October 2017

Mambo matatu ya muhimu unayopaswa kuyajua kuhusu embe

health-benefits-of-mango
Ukiamua kuzungumzia matunda yenye faida kimwili naamini huwezi kuacha kulitaja embe
Tunda hilo ambalo huzaliwa na mti ambao mara nyingi huonekana yenye ukubwa wa wastani na rangi ya kijani kibichi kila wakati.

Kabla ya kuzaliwa embe mti wake huanza kwa kuwa na maua ya rangi ya waridi hadi nyeupe katika vishada vya maua.

Tunda la embe umbo lake hutofautiana kutoka aina moja hadi nyingine, lakini mengi yao huwa aidha na rangi ya kijani, manjano ama nyekundu.

Embe inaweza kuiva ikiwa mtini lakini ili kuzuia uharibifu kutoka kwa ndege na popo ambao hula tunda hili, wakulima huamua kuvuna mara tu inapoonekana kukomaa kwa kuangusha ikiwa bado haijaiva.

Utagundua kuwa embe imekomaa kwa kuangalia rangi kwani hubadilika kutoka rangi ya kijani hadi ya manjano au nyekundu.

Zipo sifa nyingi za embe lakini kwasasa naomba nikueleze hizi  faida nyingine mbili za kula embe mara kwa mara huenda nitakufanya uanze kutumia tunda hili mara nyingi zaidi.

Embe ni moja ya tunda muhimu kwasababu husaidia kuboresha afya ya moyo kutokana na kuwa na madini ya magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo.

Madini ya magnesium husaidia kudhibiti msukumo wa damu mwilini pamoja na kushusha shinikizo la juu la damu mwilini.

Tunda hili hupunguza madhara ya tatizo la maumivu ya mifupa kutokana na kuwa na vitamin C pamoja na 'collagen' , hivyo ulaji wa tunda hili kwa wingi humuweka mhusika katika upande mzuri wa kupambana na matatizo hayo ya maumivu ya mifupa.

Mbali na hayo tunda hili linanafasi ya kupunguza madhara ya pumu kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'beta- carotene', ambacho husaidia kupunguza madhara na dalili za pumu.

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment