
Miwa ni moja ya zao muhimu ambalo hutumika katika kukamilisha uzalishaji wa sukari. Hata hivyo zipo faida kadhaa za matumizi ya juisi ya miwa kiafya.
Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuimarisha kinga za mwili, lakini pia matumizi ya juisi hii husaidia kuongeza baadhi ya virutubisho mwilini.
Aidha, juisi hii pia husaidia kwa wale wenye shida ya matatizo ya mkojo 'urinary tract infections', pamoja na kulinda afya ya figo.
Matumizi ya juisi ya miwa pia husaidia kuboresha umeng'enyaji wa chakula ndani ya tumbo na hivyo kupunguza uwezekano wa ukosefu wa choo.
Pamoja na hayo, juisi hii inamadini ambayo husaidia kulinda afya ya meno.
Kama utahitaji maelekezo zaidi kutoka kwetu basi usipate shida unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
No comments:
Post a Comment