Wednesday, 25 October 2017

Mambo yakuyafahamu kuhusu juisi ya limao na faida zake


Juisi ya limao mara nyingi imekuwa ikitumika katika kuleta ladha tofauti ya chakula au kuondoa harufu fulani ya chakula (shombo).

Mbali na tunda hilo kuwa na faida katika masuala ya kiupishi, lakini pia huweza kutumika katika  masuala mengine yakiwemo ya usafi.

Juisi ya lima hupendekezwa kwa matumizi ya watu wenye shida ya kuhisi kizunguzungu mara kwa mara hususani wale ambao kizunguzungu hicho hakitokani na upungufu wa damu mwilini.

Pia hutumika kuzuia maambukizi kadhaa pamoja na kuponya mafua na baridi, huku pia ikizuia madhara ya mawe kwenye figo.

Mbali na hayo zipo baadhi ya tafiti ambazo zinaeleza kwamba, juisi hiyo hufaa pia hata kwa wale wenye malengo ya kupunguza uzito wa mwili.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment