Monday, 9 October 2017

Matatizo 7 ya kiafya yanayoweza kusaidika kwa kutumia majani ya mpera


MTI wa mpera ni miongoni mwa miti ya matunda inayofahamika na wengi hapa nchini. Mti huu hutoa matunda yanayofahamika kama mapera, lakini leo tutaangalia faida za majani ya mti huu.

Majani hayo hayo ya mpera pia huwasaidia wale wenye matatizo ya kuharisha, ili kukabiliana na tatizo hilo mgonjwa wa kuhara huweza kuandaliwa maji yatokanayo na majani ya mpera ambayo yamechemshwa na kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Vilevile majani ya mpera husaidia kutibu tatizo la vidonda vya tumbo, huku likiwa na virutubisho vingi ambavyo husaidia kuimarisha fizi na kuongeza vitamin B na A mwilini.

Majani ya mpera yenye uzito wa kilo moja yanapopondwa na kisha mgonjwa akanywa lita moja ndani ya siku nzima husaidia kukinga seli za mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Majani mateke ya mti huo yanapofungwa shingoni kwa mwenye tezi huweza kuponyesha tatizo hilo pia na mwenye jipu akifunga sehemu husika hulifanya jipu kuiva kwa haraka.

Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibu maradhi mbalimbali , halikadhalika juisi ya mapera nayo husaidia sana kutibu mgolo au bawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katika moyo.

Kama utahitaji maelekezo zaidi kutoka kwetu basi usipate shida unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment