Wednesday, 25 October 2017

Matunda yanayoweza kukulinda kiafya yakitengenezwa kama juisi

Kuna baadhi ya vinywaji huwa tunapenda kuvitumia sana, lakini huenda huwa hatufahamu ni nini matokeo yake katika kuboresha afya zetu, miongoni mwa vinywaji hivyo ni pamoja na juisi zitokanazo na matunda mbalimbali.

Leo nimekuandalia hii orodha ya aina ya juisi na faida zake ndani ya mwili.
JUISI YA CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Mchanganyiko wa matunda haya unapotengeneza juisi husaidia kung’arisha ngozi na kuifanya kuonekana laini, huku pia ikisaidia kupunguza joto la mwili, lakini kwa wale wenye shida ya kuwa na ngozi kavu juisi hii huwasaidia sana.

JUISI YA NDIZI, NANASI NA MAZIWA
Unapopatikana mchanganyiko wa juisi ya namna hii, basi mtumiaji hupata kiasi kingi cha vitamin na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huku ikisaidia sana kuzuia tatizo la ukosefu wa choo.

JUISI YA KAROTI, EMBE, TUFAHA NA PEASI
Matumizi ya juisi hii yanaelezwa kusaidia kuzuia athari ya sumu mwilini na hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

JUISI YA KAROTI, TUFAHA NA TANGAWIZI
Mchanganyiko wa matunda haya hutoa juisi ambayo huwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Ifahamike kuwa tufani ni ‘Apple’ kwa kiingereza.

JUISI YA NANASI, TIKITI MAJI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya husaidia sana kusafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hivyo juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo na hata kujikinga na magonjwa hayo.

JUISI YA MIWA
Juisi ya aina hii inafaida sana ndani ya mwili ikiwa ni pamoja na kuupatia mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ inayopatikana ndani yake. Halikadhalila juisi hii inauwezo mkubwa sana wa kupambana na saratani hususani ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa, uwezo wake huo unaotokana na kuwa miwa ni jamii ya tunda lenye 'alkali.'

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment