Wednesday, 4 October 2017

Mbegu za maboga zinavyoweza kukupa thamani kwenye afya yako

Mbegu za maboga nazo zina faida zake ikiwa ni pamoja na kwa na kiwango kizuri cha protini na vitamin

Si kila mtu anaweza kutambua faida za mbegu hiso na ndio maana wengi wao hudharau mbegu za maboga pengine kwa kutokufahamu faida zake, lakini ni wazi kwamba mbegu hizi ni miongoni mwa mbegu zenye faida, kwani huweza kuzuia na hata baadhi ya magonjwa.

Miongoni mwa faida za mbegu hizi ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hii ni kutokana na kuwa na kiwango kingi cha madini aina ya 'magnesium', ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu.

Aidha, mbegu hizi za maboga pia zina kiwango cha madini aina ya 'zinc', ambayo faida yake mwilini ni pamoja na kuimarishaji kinga za mwili, Hali kadhalika 'zinc' huimarisha nguvu za kiume.

Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha madini ya 'zinc', tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza pia kutoa ahueni kwa watu wenye saratani ya kibofu.

Jinsi ya kutumia mbegu hizi utahitajika kupata kiasi cha mbegu za maboga kisha saga na utatumia unga huo kwa kuweka kwenye maji ya motoa ua uji. Tumia mara mbili kwa siku asubuhi na jioni

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment