Tuesday, 17 October 2017

Michanganyiko ya aina 3 ya aloe vera yanye kuondoa madoa ya chunusi


Aloe vera ni moja ya mmea ambao huwa na uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwa ni pamoja na matatizo yanayohusu ngozi.

Leo naomba kukueleza msomaji wangu namna aloe vera inavyoweza kutumiaka katika kuondoa madoa ya chunusi.

1.Aloe vera
Mmea huu unaweza kutumika wenyewe bila kuchanganywa na kitu chochote na ukasaidia kuondoa madoa hayo ya chunusi. Jambo la kufanya ni kukata kipande cha mmea huo na baadaye kutumia ute wake (utomvu) wake kugusisha sehemu zenye madoa na baadaye kunawa baada ya robo saa.

2. Aloe vera na mdalasini
Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri kwenye matumizi ya kusaidia kuondoa chunusi pamoja na madoa yake, lakini uwezo wa kiungo hiki unaweza kuwa na ufanisi zaidi pale unapongezwa na aloe vera na kisha kupaka sehemu yenye madoa.

3. Aloe Vera na Limao
Matumizi ya kijiko kimoja cha limao na kijiko kimoja cha aloe vera vinapochanganywa kwa pamoja huweza kusaidia kuondoa hali ya madoa yatokanayo na chunusi. Hakikisha hautumii mchanganyiko huu kwa kusugua sana kwani huweza kuchangia kuadili rangi ya ngozi yako na kuwa nyeupe zaidi.

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment