Thursday, 5 October 2017

Mjamzito zingatia mambo haya manne yamsingi


Habari za leo mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com leo naomba tuzungumze kuhusu mambo muhimu wakati wa ujauzito pamoja na unyonyeshaji.

Wanawake wengi wanapokuwa wakati wa kipindi cha ujauzito hujikuta wakianza kutojijali na kijiweka hovyo hovyo jambo ambo huchangia wengi wao kupoteza mvuto.

Baadhi yao hujikuta wakiendelea kuwa katika hali hiyo hata mara baada ya kujifungua na ukimuuliza kwanini atakwambia analea.

Kimsingi ni kwamba kujifungua au hali ya kuwa na ujauzito haifai kuwa sababu ya mwanamke kupoteza mvuto aliokuwanao hapo awali. Hivyo ni vizuri mwanamke unapokuwa katika hali hiyo ukahakikisha unabaki katika muonekano wako ule ule wa awali.

Kumbuka kuwa katika kipindi hiki cha ujauzito au kulea unaweza kutumia vipodozi visivyo na kemikali na ukaendelea kuonekana vizuri tu.

Zingatia kwamba wakati wa ujauzito mama hupaswi kupaka vipodozi vyenye kemikali, kwani huweza kusababisha madhara kwa mtoto.

Pia ni vizuri kutumia muda mwingi kufanya mazoezi mepesi mepesi ambayo husaidia sana kukuweka katika ‘shape’ nzuri pamoja na hali ya ujauzito ulio nao kazi ya kulea.

Mama aliyejifungua naye anapaswa kuepuka kupaka mafuta, yenye harufu kali inayoweza kuwa na madhara kwa mtoto na wakati wengine kumsababishia mtoto wakati mgumu katika kupumua.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment