Tuesday, 24 October 2017

Mpangilio wa vyakula vitakavyokusaidia kuondoa sumu mwilini mwako


Miili yetu huweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika mwilini kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mazingira tunayoishi na vyakula tunavyokula kila siku.

Sumu hizo pia huweza kutokana na matumizi ya dawa mbalimbali hususani za kizungu (kisasa) ambazo huwa tunakunywa kwa lengo la kujitibu magonjwa mbalimbali.

Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kukusaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini:-

1. Kula vyakula asili zaidi kuliko vyakula vya viwandani

2. Mlo wako mmoja kati ya milo mitatu ubadilishe na uwe wenye matunda mbalimbali pekee.

3. Jitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku, kumbuka unahitaji glasi 8 hadi 10 za maji kila siku.

4. Punguza matumizi ya chai ya rangi na kahawa.

5. Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber) kwa kiwango kikubwa zaidi.

6. Kama mazingira yanakuruhusu kutumia dawa asili, basi jitahidi kufanya hivyo zaidi.

7. Epuka matumizi ya vileo mbalimbali.

8. Jitahidi kupata muda mzuri wa kupumzika na kulala kiasi cha kutosha.

9. Punguza msongo wa mawazo

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment