Wednesday, 11 October 2017

Msaada wa chai ya mdalasini kwa wenye 'pressure'


MDALASINI ni miongoni mwa viungo vinavyotumika kuongeza ladha katika vyakula, pia kikitumika ipasavyo huweza kutoa ahuenu kwa matatizo mbalimbali likiwemo la 'pressure'.

Leo naomba nikueleze msomaji wangu namna ya kutumia mdalasini kwa wenye tatizo hilo:-

Unapotumia kiungo hiki kila siku huweza kupunguza madhara ya tatizo la pressure , kutokana na uwezo wake wa kushusha kiwango cha sumu mwilini 'cholesterol'.

Aidha, kinywaji chenye mdalasini huwa na nafasi ya kuwasaidia wale wenye shida ya kisukari pia. kutokana na uwezo wake wa kurekebisha mfumo wa uzalishaji wa insulin ndani ya mwili.

Pia kinywaji hiki husaidia kurekebisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni na hivyo kupunguza madhara ya kukosa choo na maumivu ya tumbo ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na miungurumo.

Kwa mujibu wa jarida la Clinical Nutrition linaeleza kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mdalasini hususani asubuhi huongeza zaidi manufaa yake kwa mtumiaji.

Unaweza kuandaa maji ya moto kikombe kimoja na kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini kisha tumia mchanganyiko huo kila siku asubuhi kwa mwezi mzima mfululizo bila shaka utaona mabadiliko.

Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu somo hili au kiungo hiki unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment