Wednesday, 11 October 2017

Njia 3 asili zakutumia kama unapenda urembo wa kucha

Uhaligani msomaji wangu wa www.dkmandai.com imani yangu ni kwamba unaendelea vyema kabisa.

Leo naomba tuzungumze namna ya kung'arisha kucha zako kwa kutumia njia asili pasipo kuwa na madhara yoyote.

Bila shaka wengi mnafahamu kuwa moja ya vitu vinavyoweza kumfanya mtu kuvutia hasa mwanamke ni pamoja na uzuri wa kucha zake hasa zikiwa halisi halafu zinazong'aa.

Zifuatazo ni njia zitakazong'aza kucha zako:-

1. Maganda ya chungwa
Kausha maganda kadhaa ya chungwa kisha usage na kupata unga wake halafu tumia unga huo kuchanganya na maji kidogo halafu paka mchanganyiko huo kwenye kucha na ukae nao kwa dakika 10. Pia unaweza kutumia maganda hayo kusugua kwenye kucha mara mbili kwa siku ndani ya wiki moja.

2. Juisi ya limao
Kamua maji ya lima kwenye bakuli kisha loweka kucha zako au vidole vyako kwenye juisi hiyo kwa muda wa dakika 12 na baadaye osha mikono yako,fanya zoezi hilo kadri uwezavyo, lakini usitumie njia hii kama unajeraha kwenye vidole vyako.

3. Maziwa
Unahitajika kupata maziwa ambayo si ya moto sana (vuguvugu) kisha weka kwenye bakuli halafu dumbukiza mkono wako ndani ya maziwa hayo na uache kwa dakika 15 baada ya hapo utoe kisha futa kucha zako kwa taulo safi. Fanya zoezi hilo angalau mara 4 kwa siku kwa muda wa wiki moja utaona mabadiliko.

Usisite kuwasiliana nasi kwa ufafanuzi zaidi au tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment