Tuesday, 10 October 2017

Njia za kumaliza maumivu ya viungo haraka


Kuna wakati unaweza kuamka mwili wote unauma bila kuwa na sababu ya msingi au kutokana na uchovu wa kazi zako.

Hivyo leo nataka kukwambia baadhi ya vyakula, vinywaji na viungo ambavyo vyenyewe huweza kutuliza maumivu ya mwili kwa haraka endapo utavitumia vizuri.

1 Asali
Hii huweza zaidi kutuliza maumivu ya mdomoni huenda yametokana na kujing'ata au sababu nyingine zozote za maambukizi.

2. Maji ya kunywa
Hivi unajua kitendo cha kunywa glasi 8 za maji kila siku ni moja ya njia inayoweza kukusaidia kukata maumivu ya mwili kwa haraka. Inawezekana huamini lakini nakushauri jaribu na utaona umuhimu wa maji mwilini.

3. Nanasi
Hili ni miongoni kati ya matunda ambayo huweza kutuliza maumivu kwa saa chache hususani maumivu ya tumbo au kujaa gesi.

4. Chumvi
Kiungo hiki hufahamika kama mfalme wa jikoni hiki huweza kutuliza maumivu hususani ya miguu kwa kuichanganya na maji ya uvuguvugu na kisha kuloweka miguu inayouma ndani ya maji hayo kwa dakika kadhaa.

5. Binzari/ manjano
Hiki kiungo kinaaminika nacho kuwa na uwezo mzuri wa kutuliza maumivu ya mwili kwa haraka huenda kushinda hata baadhi ya dawa unazozifahamu ni hodari za kutuliza maumivu.

6. Mafuta ya kitunguu swaumu
Mafuta haya huweza zaidi kutuliza maumivu ya sikio kwa kudondosha tone moja la mafuta hayo kwenye sikio lenye maumivu.

7. Karafuu
Ni moja ya kiungo ambacho zaidi hupatikana Zanzibar, lakini husaidia zaidi kutuliza matatizo ya maumivu ya meno kwa ujumla, lakini pia hushusha kiwango cha cholesterol mwilini.

8. Tangawizi
Kiungo hiki ni mahususi kwa kutuliza maumivu ya misuli na mifupa 'joint' na huweza kutoa majibu ndani ya mwezi mmoja tu.

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300 au zungumza moja kwa moja na Mtaalam Mandai kwa namba 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment