Monday, 2 October 2017

Sababu 4 zitakazokukufanya uanze kutumia kabeji nyekundu


Kwa hali ya kawadia wengi tumezoea kuziona na kula kabeji zile zenye rangi ya ukijani kwa mbali na ni nadra sana kukutana na kabeji zenye rangi tofauti na hiyo.


Kabeji huwa na faida mbalimbali kwa afya zetu wanadamu na huweza kutumika katika kutatua matatizo mbalimbali kutokana na  aina ya uandaaji.

Tukizungumzia kabeji ya kijani au purple kabeji, hii ni miongoni mwa aina ya kabeji ambayo haipatikani kwa wingi, lakini inafaida zake pia

Leo nimeona nikueleze msomaji wangu kuhusu faida za kabeji nyekundu (purple kabeji) katika miili yetu.

Kwanza kabisa matumizi ya kabeji hii husaidia kuboresha afya ya macho na kumfanya mhusika kuwa na nuru katika macho na kuona vizuri zaidi. Hii ni kutokana na kuwa na kiwango kizuri cha vitamin A ndani yake.

Aidha, aina hii ya kabeji kwa kiasi kikubwa inasaidia kuimarisha kinga za mwili kwasababu ndani yake kuna kiwango kizuri cha vitamin C pia.

Pia kabeji aina hii ni moja ya njia ya kutuliza madhara yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Pamoja na hayo, kabeji hii pia inauwezo wa kuwasaidia wale wenye malengo ya kupunguza uzito pamoja na wale wenye uhitaji wa kuonekana vijana kutokana na uwezo wake wa kutunza afya ya ngozi pia.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment