Monday, 16 October 2017

Sababu za kutohisi hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Tumekuwa tukipokea maswali mara kadhaa kuhusu tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa na mara nyingi maswali hayo yamekuwa yakiulizwa na kinamama ambao tayari wapo kwenye ndoa.

Hata hivyo, mara nyingi tatizo hili huweza kuchangiwa na tabia kadhaa ambazo tumekuwa tukizifanya karibu kila siku.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo huweza kuchangia tatizo hili la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanandoa:-

1. Mpangilio mbovu wa vyakula
Kuna baadhi ya vyakula vinapoliwa mara kwa mara huweza kuchangia tatizo hili ikiwa ni pamoja na vyakula vyenye mafuta mengi, lakini pia hata vyakula vyepesi vinapotumiwa mara kwa mara huweza kuwa chanzo. Hivyo kila unapokula kumbuka pia mlo wako unanafasi ya kukufanya uweze kuondokana na tatizo hili.

2. Kukosa muda wa kulala
Hii nayo ni miongoni mwa sababu ambayo huweza kupelekea hali hiyo ya kutohisi hamu ya tendo la ndoa kwa wanandoa, hivyo unapaswa kuzingatia unapata muda wa kutosha wa kulala.

3. Kukosa mazoezi
Ili mtu aweze kupata shahuku ya kushiriki tendo la ndoa anahitaji kuwa mchangamfu ambao mara nyingine hutokana na kufanya mazoezi mara kwa mara. hali ambayo pia huchangia hata mzunguko wa damu mwilini kuwa vizuri na hivyo damu kufika ipasavyo hadi kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia na baadaye kuhamasisha mwili kushiriki tendo hilo.

4. Msongo wa mawazo
Mawazo yanapozidi nayo huwa ni chanzo cha tatizo, mtu anapozongwa na mawazo kwa kipindi kirefu huwa katika hatari ya kukumbwa na hali hii kwasababu akili inakuwa imeegemea zaidi kwenye yale matatizo yanayomkabili na hata kusahau kabisa kuhusu ushiriki wa tendo hilo.

5. Kutojiamini / Hofu
Tendo la ndoa ni hali inayoendana pia katika mwelekeo wa kisaikolojia, hivyo mwili unapoonesha hofu juu ya kitu fulani basi hali hiyo pia huweza hata kuvuruga kabisa mpangilio mzima wa hisia za tendo la ndoa. Hivyo ni vyema kuondokana na hali hiyo kabisa ili kuepuka kupatwa na tatizo hilo.

Asante kwa kuendelea kufuatilia mtandao huu kwa mengine zaidi unaweza kuwasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa kwenye simu yako kutoka kwetu kila au kila mara tutakapokuwa tunapost.

No comments:

Post a Comment