Friday, 6 October 2017

Viazi vitamu vinavyoweza kuwa msaada kwa wenye kisukari

Viazi vitamu ni moja ya vyakula ambavyo vinapendekezwa kwa mama mjamzito kutokana na kuwa na sukari asili ambayo husaidai kuweka sawa kiwango cha insulin mwilin na hivyo kupambana na kisukari.

Uzuri wa viazi vitamu huwa na kirutubisho kiitwacho beta- carotene ambacho hutumika kusaidia utengenezaji wa vitamin A mwilini.

Uwepo wa kirutubisho cha beta - carotene pia huweza kutumika kama antioxidants  ambayo husaidia kupunguza madhara ya maumivu ya viungo, hulinda afya ya mapafu hivyo ni vizuri kutumiwa kwa watu wenye pumu pia.

Aidha, viazi vitamu vimesheheni nyuzinyuzi ambazo ni muhimu kwa umeng'enyaji wa chakula tumboni na husaidai kukinga dhidi ya saratani ya utumbo na ukosefu wa choo.

Pia ndani ya viazi hivi kuna vitamin D, ambayo ni muhimu kwa afya ya meno, mifupa, moyo na ngozi.

Lakini pia ndani ya viazi kuna vitamin B6 ambayo ni muhimu kwa kuulinda mwili dhidi ya matatizo ya shambulio la moyo na kiharusi.

Pamoja na hayo, viazi vitamu ni chanzo kizuri cha madini chuma ambayo husaidia uundaji wa seli nyeupe na nyekundu za damu, hivyo kufanya kuwa na uwezo wa kupambana na tatizo la ukosefu wa damu mwilini (anemia).

Mbali na hayo, ndani ya viazi pia kuna madini ya 'potassium' ambayo husaidia kuongeza mtiririko mzuri wa hewa ya oxygen mwilini na kurekebisha kiwango cha maji mwilini, huku ikisaidia kuweka sawa mapigo ya moyo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment