Thursday, 26 October 2017

Vitu 3 unayopasswa kuvifanya mwanamke mara baada ya tendo la ndoa

Tendo la ndoa ni tendo la faragha kati ya watu wawili wenye jinsia mbili tofauti yaani mwanamke na mwanaume.

Mara nyingi tendo hili limezoeleka kuanzishwa na wanaume na baadaye wanawake hufuata baada ya kuhamasishwa kufanya hivyo na mwanaume yaani mwenzi wake.

Leo nataka kuongea na wanawake kuhusu mambo matatu ya kufanya mara baada ya tendo la ndoa kumalizika/ kukamilika.

1. Kwenda haja ndogo
Licha ya hali ya uzito ambayo hujitokeza mara baada ya kukamilika kwa tendo hilo, lakini unaambiwa ni vyema mara tu mwanamke unapomaliza kushiriki tendo hilo uende kupata haja ndogo (kukojo). Hii humsaidia mwanamke endapo kunamaambukizi yoyote hususani ya bakteria hasa wa U.T.I kushindwa kufika mbali zaidi kutokana na wadudu hao kutoka kupitia njia ya haja ndogo.

Kufanya hivi humsaidia mwanamke kupunguza madhara mbalimbali yanayoweza kujitokeza endapo mwanamme atakuwa na maambukizi fulanifulani yakiwemo ya U.T.I

2. Kunywa maji mengi
Mwanamke unashauriwa kunywa maji ya kutosha mara baada ya kushiriki tendo la ndoa, kama ilivyo kwa mtu anayefanya mazoezi hivyo hivyo mtu aliyetoka kushiriki tendo hili hupaswa kunywa maji ya kutosha hali ambayo pia husaidia kupunguza madhara ya U.T.I .

3. Safisha sehemu yako ya siri kwa kutumia sabuni zisizo na kemikali
Unapofanya usafi maeneo hayo mara baada ya tendo hilo husaidia kujiweka mbali dhidi ya mammbukizi mbalimbali ya magonjwa. Jisafishe kutoka mbele kuelekea nyuma na ukumbuke si lazima usafishe hadi ndani zaidi ya sehemu zako za siri wewe fanya tu kwenye maeneo ambayo kwako yanaonekana kirahisi.

Kuhusu usafi wa ndani zaidi huo huweza kufanywa na mwili wenyewe kujisafisha kutokana na Mungu namna alivyokuumba.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandatz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment