Thursday, 26 October 2017

Vyakula 10 unavyotakiwa kula kama ngozi yako ni ya mafuta sana

Leo Alhamis naomba tuendelee kufahamishana mambo mbalimbali kuhusu afya zetu na kwa sasa naomba nikufahamishe hizi mbinu za kukusaidia kama ngozi yako hasa (uso) wako unapokuwa na mafuta mengi.

Ni ukweli kwamba unapokuwa na ngozi yenye asili ya mafuta mengi hukera kwani muda wote uso huonekana kung'aa zaidi hata kama umepaka baadhi ya vipodozi vya kuzuia uso kuwa na mafuta mengi.

Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo huweza kusaidia kupunguza hali ya mafuta usoni:-

1. Chungwa
Chungwa na limao huweza kupunguza hali ya mafuta usoni kutokana na matunda hayo kusheheni vitamin C nyingi pamoja na kutoa sumu mwilini na hivyo kutoa mafuta yasiyohitajika mwilini.

2. Mboga za majani
Mboga hizi huwa hazina kiwango cha mafuta, isipokuwa zinautajiri wa nyuzinyuzi (fiber) ambayo huweza kusafisha mafuta kwenye ngozi.

3. Parachichi
Kitu kikubwa kuhusu tunda hili ni kwamba mbali na kuliwa pekee, bali huweza kupakwa moja kwa moja kwenye ngozi na kupunguza kiwango cha mafuta usoni.

4. Ulaji wa vyakula vya nafaka
Vyakula hivi huwa na wingi wa nyuzinyuzi, ambazo husaidia kurekebisha mmeng'enyo wa chakula kuwa vizuri zaidi na kuifanya ngozi kutokuwa na mafuta mengi na hata chunusi pia.

5. Maji ya nazi
Nayo huweza kupunguza hali hiyo kutokana na kurejesha ukavu kwenye ngozi

Kuna vingine vingi ambavyo huweza kupunguza mafuta kwenye ngozi ikiwa ni pamoja na ndizi, broccol, samaki, zabibu na limao

Kama hutahitaji maelezo zaidi kuhusu mada hii naomba wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment