Saturday, 14 October 2017

Vyakula 5 vinavyopendekezwa kutumiwa kwa wenye maumivu ya mgongo

Maumivu ya mgongo huwatesa watu wengi hasa wale wenye umri mkubwa, jambo ambalo husababisha watu hao kutojisikia vizuri au kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo.

Moja ya sababu za maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya mhusika. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama huchangia sana maumivu ya mgongo hasa kwa baadaye.

Sababu nyingine inayoweza kupelekea maumivu hayo ni pamoja na ubebaji wa mizigo mizito usiozingatia afya ya mgongo na hata kulalia matandiko (magodoro) laini wakati wa kulala.

Uzito wa kupita kiasi (ujauzito, kitambi) huweza kusababisha maumivu ya mgongo pia, ila kwa kina mama wajawazito kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimama.

Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo, lakini pia kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgongo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali huweza kuwa sababu pia ya maumivu ya mgongo.

Leo ninayo orodha ya vyakula ambavyo husaidia kupunguza maumivu ya mgongo endapo vitatumika mara kwa mara.

1. Maziwa
Ni kinywaji muhimu kwa watu wenye shida ya maumivu ya mgongo kutokana na uwezo wake wa kuimarisha afya ya mifupa kwani maziwa yanavirutubisho muhimu kwaajili hiyo. Unaweza kujenga utaratibu wa kunywa glasi moja ya maziwa kila siku.

2. Samaki
Matumizi ya samaki nayo ni muhimu kwa mwenye shida hii kutokana na kuwa na omega 3, ambayo nayo huwa na nafasi ya kupunguza maumivu ya mgongo inapopatikana kiasi cha kutosha mwilini.

3. Matunda
Matunda nayo huweza kuwa msaada kwa wenye maumivu hayo, kutokana na kuwa na vitamin na madini mbalimbali ambayo huwa na uwezo wa kupunguza uwezekano wa maumivu ya aina hiyo.

4. Supu ya kuku
Ni nzuri pia kutokana na kusheheni virutubisho vingi na muhimu ambavyo navyo huweza kupunguza maumivu ya mgongo. Pia supu hii hupendekezwa zaidi kutumika kwa watu wenye umri kuanzia miaka 50 hadi 60 ambapo huwafanya kuwa na afya bora zaidi ya mifupa.

Hata hivyo ni vyema supu hiyo ya kuku ikatokana na kuku wa kienyeji na si wale wa kisasa ili kupata faida vizuri zaidi.

5. Mayai
Ulaji wa angalau yai moja kwa siku unaweza kukuhakikishia usalama wa maumivu ya mgongo kutokana na yai kuwa na virutubisho na madini yenye uwezo wa kupunguza maumivu hayo.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuongea nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment