Friday, 13 October 2017

Vyakula & matunda 5 kwa wenye shida ya upungufu wa damu

Anemia ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.

Upungufu wa damu hujitokeza pale ambapo mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu zinapopungua kupita kiwango cha kawaida.

Mtu huweza kukubwa na tatizo hili la upungufu wa damu kutokana na sababu mbalimbali ikiwa hii ya kuvuja damu kunakotokana na jeraha au kunakotokana na vipindi vya hedhi na nyakati za kujifungua pia.

Sababu nyingine inayoweza kusababisha tatizo hili ni uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini au lishe duni na vile vile magonjwa sugu au ya muda mrefu, ambapo 'bone marrow' hushindwa kufanya kazi inavyopaswa.

Leo ninayo orodha ya vyakula na matunda anayopaswa kupatiwa mtu mwenye shida hii ya anemia:-

1. Tende

2. Tunda la mtini (figs)

3. Mchanganyiko wa juisi ya tufaa na nyanya

4. Komamanga (pomegranate) 

5. Mchanganyiko wa ndizi na asali

Kwa ushauri zaidi unaweza kuongea nasi kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment