Wednesday, 25 October 2017

Vyakula muhimu kwa wanawake hivi hapa


Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu kwa ajili ya afya yako na maendeleo ya mtoto anayepo tumboni.

Zifuatazo ni dondoo muhimu za kukuwezesha uwe na lishe nzuri wakati wa ujauzito:

Kwanza hakikisha unapata mlo kamili kila siku kwa kupata vyakula vya protini, wanga, vitamin, mafuta, madini na maji ya kutosha.

Kula sana matunda na mboga za majani. Ikiwezekana nusu ya mlo wako iwe ni matunda na mboga za majani 

Tumia nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona au mtama, mchele usiokobolewa, mikate ya brown.

Chagua vyanzo vyako vya protini zaidi katika samaki, kuku, mayai, jamii ya maharage, soya na karanga.

Kunywa maji yakutosha kila siku, zisipungue lita 2.5 kwa siku.

Mazoezi pia ni muhimu, unaweza kutembea kwa dakika 30 kwa siku.

Acha au epuka matumizi ya pombe kwani huathiri afya ya mtoto tumbo

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment