Saturday, 21 October 2017

Yafahamu mafuta yenye uwezo wa kutuliza vidonda vya tumbo


Kuna mafuta mbalimbali ambayo tumekuwa tukitumia katika uandaaji wa vyakula vyetu vya kila siku.

Lakini leo naomba tuzungumzie kuhusu mafuta ya mzaituni ambayo nayo yanafaida zake hasa kwa wenye vidonda vya tumbo.

Mzaituni ni mti unaostawi katika mataifa mbalimbali duniani, lakini zaidi huweza kustawi zaidi nchini Israel.

Mti huu ambao umetajwa mara kadhaa katika vitabu vya dini pia unaelezwa kuwa na uwezo wa kutoa ahueni kwa matatizo kadhaa ya kiafya.

Mafuta hayo huwa na manufaa mbalimbali kiafya, lakini leo napenda kukufahamisha kuwa mafuta ya mzaituni huweza kupunguza madhara ya vidonda vya tumbo.

Mafuta hayo huweza kupambana na tatizo hilo kutokana na kuwa na uwezo wa kupambana na aina mbalimbali ya bakteria na miongoni mwa bakteria ambao huweza kdhurika na mafuta haya ni pamoja na bakteria aina ya 'Helicobacter Pylori', ambao huishi tumboni na husababisha tatizo la vidonda vya tumbo.

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment