Monday, 30 October 2017

Zifahamu faida za karoti zinapochanganywa na viungo vingine


Karoti ni moja ya kiungo/ tunda ambalo wengi tunakifahamu na huwa tunatumia kwa kuweka kwenye baadhi ya vyakula kwa lengo la kuongeza ladha na mvuto wa rangi ya chakula.

Karoti imesheni virtubisho vingi na muhimu na madini ambavyo vyote kwa pamoja hutusaidia sana kutukinga na kutibu dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya uoni hafifu, ngozi, nywele na kucha.

Tunda hili pia husifika kwa uwezo wake wa kuimarisha afya ya ngozi kutokana na kuwa na vitamin A kwa wingi, ambayo husaidia kujenga afya ya mwili.

Unywaji wa juisi ya karoti kila siku ni mzuri na ni vyema ukafanya hivyo kama unaweza hii ni kutokana na faida za juisi hiyo kiafya ambazo nitaziorodhesha hapa chini:-

Miongoni mwa faida za juisi ya karoti ni pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Pia juisi hii inasifika kwa kuongeza uoni mzuri kwa mtumiaji kwani husaidia sehemu ya ndani ya jicho (retina) kuwa vizuri zaidi kutokana na kuwa na virutubisho vya 'lutein' na 'beta -carotene' .

Aidha, juisi hiyo pia husaidia kurekebisha kiwango cha sukari ndani ya mwili na kushusha kiwango cha sumu mwilini (cholesterol).

Uwepo wa mchanganyiko wa tangawizi ndani ya juisi ya karoti ambapo hufanya kinywaji hicho kuwa suluhisho la matatizo ya kukatika kwa nywele na kuzifanya kuwa imara zaidi.Hivyo ni juisi nzuri kwa wanawake wanaopenda urembo wa nywele.

Mchanganyiko huo pia hutumika kama kinga dhidi ya saratani, matumizi ya juisi ya karoti yenye mchanganyiko wa tangawizi husaidia kuukinga mwili dhidi ya matatizo ya saratani za aina mbalimbali kwani husaidia kuua seli zinazoweza kuchangia matatizo ya saratani.

Hulinda meno na fizi, karoti pekee yake kwanza inatosha kwa kuwa mlinzi mzuri wa kinywa, hivyo matumizi ya glasi moja ya juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi baada ya kula husaidia pia kulinda afya ya kinywa kwa ujumla.

Mtaalam wa lishe tiba, Abdallah Mandai anaeleza kuwa, matumizi ya juisi ya karoti nayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na kumlinda mhusika dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya macho, kutokana na karoti kuwa na vitamin A ya kutosha.

Pamoja na hayo, mtaalam huyo anaongeza kwamba, juisi hiyo ya karoti inasifika kwa kuimarisha mifupa, kutokana na kuwa na madini ya ‘potassium’ ambayo hupatikana ndani yake.

Sambamba na hayo, Mandai anasema namna mchanganyiko wa matunda ya aina tatu yaani matikitimaji, tufaa (apple) pamoja na karoti ambavyo huweza kujenga na kuimarisha kinga za mwili endapo yataandaliwa vizuri.

Matunda hayo kwa pamoja yatahitajika kuandaliwa vizuri kwa kuyaosha na kutoa maganda pamoja na mbegu na kisha kuchanganywa kwa pamoja na baadaye kusagwa, huku ukianza na tufaa na matikitimaji na baadaye kuchanganywa kwa pamoja na karoti iliyosagwa .

Baada ya mchanganyiko huo kusagika unashauriwa kuchuja mara moja na kuweka kwenye jagi na baadaye kuongeza kiwango kidogo sana cha sukari au kutoweka kabisa, kisha utatumia mchanganyiko huo kunywa asubuhi na jioni kila siku kikombe kimoja . Fanya zoezi hilo angalau kwa miezi miwili mfululizo na itakusaidia katika kukukinga dhidi ya magonjwa ya mara kwa mara.

Kama unaswali, maoni au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

1 comment: