Wednesday, 31 January 2018

Mazoezi ya viungo yanasaidia kuyepuka kisukari

UGONJWA wa kisukari ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza ambao unawakumba watu wengi zaidi nchini na duniani kote hasa nyakati hizi.
Ugonjwa huu unatokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushaji chakula ndani ya mwili wa binadamu. Watu wanaopenda anasa na starehe bila kuzingatia kufanya mazoezi, wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na kisukari.
Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema idadi ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ulimwenguni imeongezeka kutoka milioni 108 mwaka 1980 hadi milioni 422 mwaka 2014.
Kisukari ni ugonjwa unaongezeka kwa kasi katika nchi zenye kipato cha kati na cha chini huku idadi kubwa ya wagonjwa wake wakikumbwa pia na upofu, kushindwa kufanya kazi kwa figo, shambulizi la moyo, kiharusi na kukatwa miguu.
WHO inasema nusu ya vifo vyote vinavyotokea kabla ya umri wa miaka 70 duniani, vinachangiwa na ugonjwa huo huku ikikisiwa kuwa ifikapo mwaka 2030, kisukari kitashika nafasi ya 7 kwa kusababisha vifo.
Ugonjwa wa kisukari unaweza kutibiwa na madhara yake kuepukika kwa kuzingatia lishe bora, mazoezi, dawa na upimaji wa sukari kwenye damu mara kwa mara pamoja na kutibu madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
Hata hivyo matibabu  ya ugonjwa wa kisukari yanamsaidia mgonjwa kuweza kuishi maisha ya kawaida kwa kuwa  yanaendelea katika kipindi chote cha uhai wake.
Miongoni mwa dalili  kuu za ugonjwa wa kisukari:
Kukojoa mara kwa mara
Daima kujisikia hamu ya kula
Kuwa na uchovu wa mwili na akili
Kiu isiyo ya kawaida
Mwasho wa ngozi ya mwili
Kupungua uzito wa mwili
Ni vema jamii ikazingatia kufanya kazi za kutumia nguvu au kufanya mazoezi ya viungo vya mwili ambayo yanasaidia kuwaepusha na kisukari.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalamu Mandai kwa simu namba +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800  au email dkmandaitz@gmail.com. Endelea kutembelea website yetu www.dkmandai.com kila siku utapata elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu afya yako.No comments:

Post a Comment