Tuesday, 27 February 2018

Afya ya Kamanda Mkumbo ina imarika –daktari


     Gari alilokuwa akisafiria kamanda Charles Mkumbo

Wankyo Gati, Arusha

HALI ya afya ya Kamanda  wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo imeendelea kuimarika baada ya kupata matibabu katika hosptali ya mkoa ya Mt Meru.

Mganga mkuu mkuu wa mkoa wa Arusha, Jackline Urioh amesema hali yake inaendelea vizuri ukilinganisha na jana baada ajali aliyopata mkoani Manyara.

“Alipata majeraha mkononi na kichwani hali yake inaendelea vizuri kwa sasa lakini bado ana maumivu makali.

Jana akithibitisha kutokea ajali hiyo jana kaimu kamanda  wa polisi  mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema ilitokea majira ya saa 10 alasiri wakati Kamanda Mkumbo akitokea mkoani Singida akiwa kwenye gari la polisi lenye namba za usajili PT 2040.

Amesema licha ya kamanda Mkumbo wengine walioumia katika ajali hiyo ni pamoja na dereva na mlinzi wake ambao hakuwataja majina lakini alisema wamepata majeraha kidogo sehemu mbalimbali za miili yao.

Kwa mujibu wa Kamanda Ilembo dereva alikuwa anaendesha gari mwendo wa kawaida lakini kwa bahati mbaya lilipasuka gurudumu la nyuma na kusababisha liache njia na kupinduka mara kadha.

Amesema baada ya ajali hiyo kutokea majeruhi hao walisaidiwa na wananchi wenye mapenzi mema na baadaye walikimbizwa katika hosptali ya mkoa ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu.


No comments:

Post a Comment