Friday, 2 February 2018

Buriani Kingunge


MWANASIASA mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia leo.
Akithibitisha kifo cha baba yake muda mfupi uliopita, mtoto wa marehemu Ton Ngombale Mwiru, amesema baba yake amefariki saa 10 alfajiri ya kuamkia leo.
Amesema familia imepokea kifo cha baba yake kwa fadhaha kubwa baada kuwa ndani  ya mwezi mmoja imeondokewa na mihimili mikuu miwili.
"Kwa ujumla familia imegubikwa na majonzi mazito hasa ukizingatia kuwa tumepoteza nyenzo zetu zote kwa maana ya baba na mama ndani ya kipindi cha mwezi mmoja" alisema Ton.
Ton alifafanua kuwa baba yake aling'atwa na mbwa miezi mitatu iliyopita baada ya hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu lakini baadaye mama yao alifariki dunia karibu mwezi mmoja uliopita ambapo madaktari walimpa ruhusa ya muda baba yake kwenda kuzika mkewe na kisha alirudishwa tena hospitali.
"Baada ya kifo cha mama hali ya baba ilikuwa ikibadilika mara kwa mara hadi saa 10 alfajiri ya leo alipofariki dunia. saa 10 .

No comments:

Post a Comment