Monday, 26 February 2018

DC ataka wakazi Dodoma kuweka mazingira safi


Deogratius Ndejembi

Mary  Meshack, Dodoma
WAKAZI  wa mji wa Dodoma wametakiwa kujenga  tabia ya kupenda usafi kwa kusafisha mazingira yanayowazunguka ili yawe safi kila wakati 
Kaimu mkuu wa wilaya ya Dodoma, Deogratius Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati wa kufanya usafi wa mazingira na upandaji wa miti uliofanyika katika mtaa wa NHC mjini hapa.
Katika mchakato huo uliodhamiwa na Mtandao wa wapenda Maendeleo na Kutetea Haki za Wanawake na Vijana Tanzania (Tagedo) ulifanyika kwenye shule ya sekondari Dodoma.
                                                
Ndejembi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kongwa amesema kama wenyeji watapenda na kujenga tabia ya usafi, hata wageni wanaohamia Dodoma katika ujio wa makao makuu ya nchi wataikuta hali hiyo nao watazoea kufanya hivyo.
Ametoa mwito kwao wa kujenga tabia ya kupanda na kuifuatilia miti ili kuhakikisha inastawi na inakua vizuri ili kufikia malengo ya kuifanya  Dodoma kuwa ya kijani ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoizindua mwaka huu ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Awali mwanzilishi wa Tagedo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Mwalimu Nyerere, Venance Kalumanga amesema mradi huo wa kufanya usafi na upandaji miti ulianza tangu mwaka jana ambapo mkoa wa Dodoma peke yake umeshapandwa zaidi ya miti 6,000.

No comments:

Post a Comment