Friday, 16 February 2018

Dk Slaa, Mboweto wala kiapo
Rais John Magufuli (kulia), akipeana mikono na balozi Dk. Wilbroad Slaa muda mfupi uliopita


RAIS Dk. John Magufuli amemwapisha Muhidin Mboweto kuwa Balozi Tanzania nchini Nigeria, na Dk. Wilbroad Slaa kuiwakilisha Tanzania nchini Sweden.

Mabalozi hao wameapishwa muda mfupi uliopita asubuhi hii Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya kula kiapo kila mmoja wao ameahidi kutumia busara, akili na maarifa kutekeleza majukumu makubwa aliyopewa na Rais akizingatia viapo alivyokula baada ya kuapishwa.

Pia kila mmoja amemshukuru Rais kwa kumwona na kumteua katika nafasi hiyo kubwa, hivyo fadhila watakayolipa ni kulitumikia taifa kwa weledi mkubwa hasa wakati huu nchini inapokuwa katika mchakato wa kuelekea katika uchumi wa viwanda.

“Nakushukuru kwa kuniteua nishike nafasi hii adhimu, niahidi kama niliavyoapa nitafanya kazi kwa bidii na weledi, nitatekeleza kazi hii kwa uaminifu na weredi mkubwa,”amesema Balozi Mboweto.

“Mh. Rais mimi nakushukuru kwa kunithamini kwa kunipa kazi hii ya ubalozi, kama nilivyoapa mheshimiwa Rais sitakuangusha, nakushukuru sana kwa heshima uliyonipa nilitumikie taifa kwa nafasi hii,”Amesema Balozi Dk. Slaa.

No comments:

Post a Comment