Monday, 19 February 2018

Fahamu aina sita ya dawa zinazosaidia kupambana na maradhi ya vidonda koo


VIDONDA vya kooni mara nyingi hutokea mtu anapokuwa ana mafua.
Mgonjwa huanza kusikia maumivu kooni, kukereketwa, baridi pamoja na kukwaruza sauti.

Tatizo hilo linaweza kukomeshwa kwa dawa za aina mbalimbali ikiwemo magome ya mwembe, ukwaju, mdalasini, bizari na chumvi.

Gome la mwembe
Chukua nusu kilo ya gome la mwembe ponda na chemsha katika lita moja ya maji, sukutua mdomoni asubuhi, mchana na jioni wakati huo kiasi kidogo cha maji hayo hakikisha unakimeza. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku tano.

Ukwaju
Tengeneza juisi nzito ya tunda la ukwaju, kunywa polepole nusu glasi mara tatu kwa siku. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku tatu hadi nne.

Mdalasini
Chemsha kijiko kimoja cha chai cha unga wa mdalasini katika glasi moja ya maji, ongeza robo kijiko cha chai ya pilipili manga na kijiko kimoja cha mezani cha asali, koroga vizuri na kunywa. Tiba hii ni ya siku tatu kunywa mara tatu kwa siku.

Mbegu za methi
Chukua vijiko viwili vya mezani vya mbegu za methi, chemsha polepole katika nusu lita ya maji kwa muda wa dakika 20, kisha chuja na kunywa maji yote baada joto kupungua, kunywa mara mbili kutwa kwa muda wa siku tatu.

Hina
Chukua kiganja kimoja cha majani ya hina, chemsha katika lita moja ya maji kwa muda wa dakika 15, baada ya maji kupoa sukutua mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu.

Bizari na chumvi ya mawe

Chukua kijiko kimoja cha mezani cha bizari, chemsha na glasi moja na nusu ya maji kwa muda wa dakika 10, ongeza chumvi ya mawe, sukutua mara nne kwa siku kwa muda wa siku tatu.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment