Thursday, 15 February 2018

Fahamu maajabu ya kitunguu swaumu na tangawizi kwa tiba ya sikio
     Mtaalamu wa tiba tishe na virutubisho, Abdallah Mandai akifafanua             namna kitunguu swaumu na tangawizi vinavyoweza kukabiliana na               maumivu ya sikio.


SIKIO kama vilivyo viungo vingine katika mwili wa binadamu, lina umuhimu mkubwa, hivyo inapotokea limekumbwa na tatizo la aina yoyote, mwanadamu hawezi kutekeleza ipasavyo kazi zake za kila siku.

Sikio, pua na koo ni viungo vyenye uhusiano wa karibu ambapo kila kimoja kinapokumbwa na tatizo kwa maana ya kupata maumivu huathiri vingine pia.

Kwa maana hiyo, pua zinapoziba, masikio na koo navyo huathirika. Maumivu ya sikio yanaweza kusababishwa na sababu mbalimbali wakati mwingine jipu linaweza kujitokeza ndani na kuwa ndiyo sababu.

Pia maumivu yake yanaweza kusababishwa na kelele za nguvu, kupenga kamasi kwa nguvu au kukaukiana ndani ya sikio.

Maumivu ya sikio yanaweza kupoa baada ya kutumia viungo au vyakula mbalimbali tunavyostawisha wenyewe katika jamii zetu kama kitunguu swaumu, kitunguu maji, karafuu na tangawizi.

Kitunguu swaumu
Andaa dawa tiba hii kwa kuponda punje mbili za kitunguu swaumu, ongeza maji kijiko kimoja cha mezani changanya vizuri kisha chukua matone matatu hadi matano weka ndani ya sikio linalouma au lililoziba. Fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tano.

Kitunguu maji
Tengeneza juisi ya kitunguu maji, weka matone matatu hadi matano katika sikio, fanya hivyo mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tano. Tiba hii ni kwa ajili ya sikio linalouma au ambalo limeziba kwa kujaa nta.

Karafuu
Chukua unga kidogo wa karafuu, changanya na kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya ufuta, weka matone matatu ya mchanganyiko huu katika sikio mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tano.

Tangawizi
Tengeneza juisi ya tangawizi, chukua matone matatu hadi matano weka ndani ya sikio mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tano. Ni vema kutambua kuwa tiba hizi pia ni kwa ajili ya sikio linalowasha.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya ikiwemo ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila Jumatatu.No comments:

Post a Comment