Monday, 12 February 2018

Fahamu mambo sita ya kuzingatia unapokabiliwa na upungufu wa damu
TATIZO la upungufu wa damu linawapata watu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupoteza damu nyingi wakati wa ajali, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbalimbali ya seli.

Pia mjauzito anaweza kukabiliwa na tatizo la upungufu wa damu, mwenye tatizo la kutokwa na hedhi nzito, kurithi tatizo katika ukoo, magonjwa sugu na lishe duni yenye ukosefu wa madini ya foliki, chuma na vitamin B12.

Hata hivyo, ni vema mtu anayekabiliana na tatizo hili azingatie kula zabibu, mchicha, bitiruti/letusi, vitunguu maji, soya na asali.

Zabibu
Ili kuongeza damu ndani ya mwili tumia juisi ya ya zabibu zilizokaushwa kwa muda wa wiki tatu.

Mchicha
Tumia juisi ya mchicha nusu glasi kila baada ya mlo wa asubuhi, mchana na jioni. Baada ya wiki mbili nenda hospitali ukapimwe kiwango chako cha damu.


Bitiruti/Letusi
Kunywa glasi moja ya juisi ya bitiruti nyekundu au letusi kwa muda wa wiki mbili, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.

Vitunguu maji
Kachumbari ya vitunguu maji ikitumiwa kila siku kwa muda wa wiki tatu inasaidia kuongeza damu.

Soya
Maharagwe ya soya ni chanzo kizuri cha damu, tumia soya katika chai, uji na hata katika ugali kwa muda wa wiki tatu.

Bizari/asali
Chukua kijiko kimoja cha chai cha bizari mbichi, changaya na kingine cha mezani cha asali, kunywa mara mbili kwa siku katika kipindi cha wiki mbili utaona mabadiliko makubwa.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kuvurugika hedhi anakaribishwa makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri au kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili ili kuuepusha na magonjwa

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.

No comments:

Post a Comment