Monday, 5 February 2018

Fahamu njia tano zinazoondoa tatizo la kukosa usingizi


KUKOSA usingizi limekuwa ni tatizo kubwa katika jamii ambalo huwapata makundi mbalimbali ya watu licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa wenye kipato kinachoridhisha wanakabiliwa zaidi na tatizo hilo.

Watu wengi tunaoshi nao wanalalamika kukosa usingizi au kupata usingizi mapema kisha kuzinduka muda mfupi na kuendelea kubaki macho (bila usingizi).

Zipo sababu nyingi zinazochangia hali hiyo, kubwa ni msongo wa mawazo unaotokana na wasiwasi, hamaniko, udhia, kufanyakazi kupita kiasi, matarajio ya baadaye, kushiba sana, kuvuta sigara, unywaji chai au kahawa nyingi au njaa.

Ili kuondoa tatizo la kukosa usingizi ni vema kuyarekebisha yalitajwa kwa kutumia vifuatavyo ambavyo vinaweza kusaidia kuliondoa.

Kwanza ni vema kabla ya kwenda kulala kunywa glasi moja ya maziwa ya uvuguvugu yaliyoongezwa kijiko kimoja cha mezani cha asali.

Pia unaweza kuchukua kikombe kimoja cha maji ya uvuguguvugu ongeza vijiko viwili vya chai vya asali koroga vizuri na kunywa polele kabla ya kwenda kulala. Asali ni dawa ya kubembeleza usingizi na kuufanya mwili uburudike.

Njia nyingine unayoweza kuitumia ili kupata usingizi ni juisi ya letusi ichanganye na mafuta ya maua rozi, paka kwenye paji la uso. Letusi ina dawa inayoitwa lektakariamu inayoburudisha mwili na kuleta hali ya usingizi.

Mtindi nao unafaa kwa kuwezesha mtu kupata usingizi. Kabla ya kwenda kulala kunywa glasi moja ya maziwa ya mtindi na uupake kwenye paji lote la uso.

Glasi moja ya juisi ya seleri changanyaji na kijiko kimoja cha mezani cha asali kunywa kabla ya kwenda kulala inasaidia sana kupatikana usingizi.

No comments:

Post a Comment