Monday, 5 February 2018

Fahamu nyenzo sita unazoweza kutumia kupambana na maumivu ya jipu
Juisi ya karela
Kitunguu swaumu


Miongoni mwa nyezo zinazosaidia kupambana na jipu (majipu)JIPU ni kijivimbe chekundu ambacho kinajaa usaha mara nyingi kinakuwa na maumivu makali.

Sehemu ya njano au nyeupe katikati ya uvimbe inaweza kuonekana wakati jipu likiwa tayari kutoa au kutokwa usaha.

Mara nyingi jipu linasababishwa na vijidudu vinavyojulikana kama stafilokokasi ambavyo vinaingia katika vijimfuko vya jasho kupitia vinyweleo.

Jipu ni uvimbe unaoanza katika sehemu maalum, linaweza kuwa moja au zaidi. Uvimbe huo unaweza kuendelea kukua hatimaye kutunga usaha na kutumbuka au kutumbuliwa.

Wakati jipu linapoanza linaweza kuonesha uvimbe unaowasha kisha kuwa na maumivu makali hasa lile linalokuwa katika sehemu ya ngozi iliyobana kama kwenye pua, sikio au kwapani.

Majipu yanaweza kuwepo pia sehemu za usoni, shingoni, makalioni, mapajani au nyingine yoyote katika mwili wa binadamu.

Chanzo kikubwa cha jipu ni sumu ndani ya mfumo wa damu inayosababishwa na kutokula chakula kinachostahili.

Hata hivyo, unaweza kutumia matunda, viungo na dawa asili kuondokana na jipu au majipu mwilini ambayo ni bizari, kitunguu swaumu au maji, muarobaini, tambuu, karela na maziwa.

Chukua kikonyo cha bizari kioke hadi kikauke kiwe cheusi kama mkaa kisha yeyusha mkaa huo ndani ya nusu glasi ya maji na paka kwenye jipu mara kwa mara, endelea kuliosha hadi lipone.

Au juisi ya kitunguu swaumu au maji,  paka kwenye jipu kwa mara. Jipu linaiva mapema na kupasuka, endelea kuosha kidonda na kupaka juisi kitapona mapema zaidi.

Pia unaweza kuponda majani ya muarobaini, bandika katika jipu, endelea kufanya hivyo jipu linapopasuka, safisha kidonda na kuendelea na tiba hadi jipu linapopona.

Si hivyo tu, unaweza pia kutumia tambuu. Paka jipu mafuta ya nyonyo, bandika jani lake juu ya jipu endelea hivyo hadi jipu linapopasuka, usiache kupaka maji ya kitunguu swaumu kila baada saa nane, fanya hivyo hadi kidonda kipone.

Jambo jingine tengeneza glasi moja ya juisi ya karela kwa kutumia matunda matatu, kisha ongeza kijiko kimoja cha mezani cha juisi ya ndimu, mgonjwa anywe pole pole asubuhi kabla hajala chochote kadhalika arudie jioni kabla ya mlo wa usiku.

Ni vema mtu aliyepatwa na jibu aendelee na tiba hii kwa muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kinga  ya kutopata majipu ya mara kwa mara.

Kijiko kimoja cha mezani cha maziwa changanya na kingine cha chai chenye siki na nusu kijiko ya cha chai cha unga wa bizari changanya vyote, paka kwenye jipu kila baada ya saa tatu, baada ya jipu kutumbuka endelea kufanya hivyo hadi kidonda kipone.No comments:

Post a Comment