Wednesday, 7 February 2018

Fanya haya kuondokana na tatizo la kukosa hamu ya kula

KUKOSA hamu ya kula chakula ni tatizo ambalo chanzo  chake ni hitilafu ndani ya mfumo wa uyeyushaji chakula katika utumbo.

Tatizo hili pia linaweza kusababishwa na msongo wa mawazo,wasiwasi, msongo wa hali ya juu wa maisha na mazingira yasiyoridhisha.

Kutokana na tatizo hilo mwathiriwa anaweza kufanya mazoezi au kutumia kitunguu swaumu kuondokana nalo.

Mazoezi
Mazoezi ya kutosha yanahamasisha uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo na kuchochea hamu ya kula chakula.  Mtu mwenye tatizo hilo ni vema afanye mazoezi kila siku kwa muda usiopungua dakika 20 au zaidi.

Kitunguu swaumu
Tafuna punje za kitunguu swaumu kila siku, kiungo hiki kinasaidia kurekebisha mfumo wa uyeyushaji wa chakula na kuleta hamu ya kula.
Kwa mwenye tatizo hilo na mengine ya kiafya anaweza kuja makao makuu yetu Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Abdallah Mandai kwa ushauri wa namna ya kutumia virutubisho na mimea kukabiliana na changamoto za maradhi mbalimbali.
Mtaalamu Mandai anapatikana kwa +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800 au dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.

No comments:

Post a Comment