Monday, 12 February 2018

Fanya haya unapobaini umeingiza sumu mwiliniKITU chochote kinachoingia katika mwili wa binadamu na kusababisha kuumwa au kufa ni sumu.

Kutokana na hilo mara nyingi binadamu amekuwa makini na vitu anavyokula, kupaka mwilini au kunywa ili asiingize sumu inayoweza kumsababishia madhara.

Sumu pia inaweza kuingia mwilini kwa kuvuta hewa, kuliwa kupitia vyakula vyetu vya kila siku, kupakwa au kugusa ngozi.

Njia inayoweza kupunguza sumu inayoingia mwilini katika mwili wa binadamu kwa njia ya chakula au kinywaji ni kutapika, kuharisha au kula chakula chenye uwezo wa kupunguza au kuondoa kabisa sumu mwilini.
Baadhi ya tiba zinazoweza kupunguza au kuondoa kabisa sumu mwilini ni haradali na mkaa.

Haradali
Chukua kijiko kimoja cha mbegu ya haradali, weka ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa ambapo baada ya dakika tano hadi 10 utaanza kutapika. Ni vema unapoabaini umeingiza sumu mwilini nenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Mkaa
Chukua vijiko viwili vya mezani vya unga wa mkaa, koroga katika glasi moja ya maji moto na baada ya kupoa kunywa. Endelea na tiba hiyo mara tatu kwa siku muda wa siku tatu. Tiba hii ifanyike sanjari na unywaji wa maji mengi iwezekanavyo.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya ikiwemo ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri au kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila Jumatatu.


No comments:

Post a Comment