Thursday, 15 February 2018

Fanya haya unapobaini una tetekuwanga
TETEKUWANGA ni ugonjwa unaowashambulia watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kama ulivyo ugonjwa wa surua.

Ugonjwa huu unaambukiza kwa haraka hasa wakati unapokuwa unaonekana unapona.

Dalili za tetekuwanga
Mara nyingi dalili za ugonjwa huu mgonjwa atajisikia mwenye homa, kuumwa na kichwa, uchovu wa mwili, kuota upele kifuani au sehemu ya juu ya mgongo unaofanana na malelege ambao unasambaa mwili mzima.

Baada ya siku chache upele huo hutumbuka na kuanza kukauka. Mgonjwa hupona katika siku 10 hadi 20. Tetekuwanga ni ugonjwa unaoenea kwa njia ya virusi.

Zipo tiba za aina nyingi za ugonjwa huu ikiwemo asali, giligiliani na karoti, chachu ya kusindikia mikate na siki ya kahawia.

Asali
Ili kusaidia kupona vidonda vya upele unaotokana na tetekuwanga paka asali mwili mzima, endelea kufanya hivyo kwa muda wa siku tatu utaona mabadiliko makubwa.

Giligilani/karoti
Chukua gramu 60 za giligilani na nyingine 100 za karoti, ponda pamoja, kisha ongeza maji lita moja, chemsha kwa dakika 10 kisha chuja na kunywa maji yote kwa siku moja. Endelea na tiba hiyo kwa muda wa siku nne.

Chachu ya kusindikia mkate
Chukua kijiko kimoja cha mezani cha chachu ya mkate, weka katika glasi moja ya maji, changanya vizuri kisha paka mwili wote wa mgonjwa kwa mchanganyiko huo ili kukausha upele na kuzuia kujikuna

Siki ya kahawia
Chukua nusu glasi ya siki ya kahawia changanya na maji ya uvuguvugu yanayotosha kumwogesha mgonjwa, mwogeshe kwayo. Endelea kufanya hivyo kwa muda wa siku tatu au nne inasaidia kuzuia kujikuna.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote mwenye tatizo au anahitaji ushauri wa kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila Jumatatu.
No comments:

Post a Comment