Thursday, 22 February 2018

Fanya haya uondokane na tatizo la kutokwa damu puani


                Mtu mwenye tatizo la kutoka damu puani

MATUKIO ya kutoka damu puani yamekuwa ya kawaida, mara nyingi ugonjwa huu unasababishwa na mipasuko midogo ya mishipa ya damu ya ndani ya pua inayosababishwa na kujeruhiwa, hali ya juu ya msukumo wa hewa, mzio au madhara yatokanayo na dawa.

Uchunguzi ambao umefanywa na wataalamu wa tiba huko Italia unaonesha kuwa kiwango cha watu kuvuja damu puani ni kikubwa wakati wa asubuhi na alasiri na ni kidogo wakati wa mchana na usiku.

Licha  ya kuwa tatizo hilo halina maelezo kamili ya chanzo chake, watu wenye msukumo wa juu na wa chini wa damu wana nafasi kubwa ya kukumbwa na tatizo hilo.

Zipo tiba asili zinazosaidia tatizo hili ambazo ni kuziba pua, ndimu na majani au mbegu ya mwembe.

Kuziba pua

Unapobaini kuwepo dalili ya kutoka damu puani hakikisha unafinya pua zote kwa vidole kwa muda wa dakika 10, ukiwa unapumua kwa mdomo na wakati huo bila kuruhusu hewa kupita puani.

Ndimu

Hali kadhalika unapoona dalili ya kutoka damu puani kwanza osha utosi wa kichwa na maji baridi, mpe mgonjwa maji mengi baridi ya kunywa mlaze chali.

Kata kipande cha ndimu, weka matone matano ya maji ya ndimu katika kila pua. Hakikisha mbegu za ndimu haziingii puani.

Majani/mbegu ya embe

Chukua majani na mbegu za embe, tengeneza juisi, mlaze mgonjwa chali, weka matone ya juisi hiyo katika kila pua. Nusu glasi ya juisi ya majani au mbegu ya embe ikinywewa ni dawa nzuri ya kuanzia kutoka damu puani.

Mada hii imeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
No comments:

Post a Comment